Lazima nikiri kwamba kuna raha ya kumuona H.Baba jukwaani zaidi ya kumsikiliza. Ni msanii ambaye ana uwezo wa kumiliki jukwaa na kwenda sambamba na mashabiki kwa nia ya kuwaburudisha. Lakini katika wimbo huu, H.Baba anasikilizika na ana ujumbe ambao unaeleweka vyema. Tubebane ndio jina la wimbo.
Kama umeshawahi kuwa kwenye mapenzi, bila shaka utakiri kwamba bila kubebana, wote mtaanguka. Pengine hili linatokana na ukweli kwamba hakuna binadamu aliyekamilika. Nipe nusu yako nami nikupe nusu yangu. Tubebane sisi wenyewe. Msikilize hapa