Sijui kama nikisema baada ya kimya cha muda fulani Nakaaya is back nitakuwa nimepatia au nimekosea. Kumbukumbu za haraka hazinijii kwamba mara ya mwisho aliachia single lini. Yote tisa. Kumi ni kwamba Nakaaya yupo tena hewani. Wimbo wake mpya huu hapa. Unaitwa Utu Uzima Dawa.
Yes ukikua na kuelewa kwamba wewe sasa ni mtu mzima na hivyo inabidi ufanye mambo yako kwa kutumia akili zako mwenyewe na sio kwa kutegemea “maisha ya kutengenezewa” basi hiyo ndio dawa. Ndio maisha na ndio utu uzima.
Hii ni production kutoka Fishcrab na Mandugu Digital.Usikilize.