Quantcast
Channel: Bongo Fleva – Bongo Celebrity
Viewing all articles
Browse latest Browse all 180

“Migulu Pande”-Madee (Audio)

$
0
0

madee migulu pande

Kuna siku niliwahi kumuulizia msanii fulani wakati wa mazungumzo yangu ya kawaida na Professa Jay(Mbunge wa Mikumi-CHADEMA). Niliuliza, “Hivi jamaa kaacha muziki au?”. Professa akanijibu kwa kifupi, “Hapana, yeye ndio muziki umemuacha”. Kwa mara ya kwanza nikawa nimetambulishwa katika dhana ya mtu kuacha muziki na muziki kumuacha yeye. Ni vitu viwili tofauti.

Kwanini nimeanza kwa utambulisho huo? Madee ni miongoni mwa wasanii ambao hawajaacha muziki na muziki haujamuacha. Alikuwepo na bado yupo. Vijana wengi wamepitia katika himaya yake. Ni jambo la kufurahisha.

Huu hapa ni wimbo wake alioutoa hivi karibuni. Migulu Pande. Sijauelewa sana lakini kuna mengi ambayo siyaelewi siku hizi. Usikilize hapa chini. (Audio Source: DJ Choka)


Viewing all articles
Browse latest Browse all 180

Trending Articles