Kuna vipaji na kisha kuna vipaji.Kila siku vinaibuka vipya. Ndio maisha na ndio hali halisi.Upende usipende. Ni mipango ya Mwenyezi Mungu.
Miongoni mwa vipaji ambavyo naviona kabisa ni pamoja na hiki cha msanii mpya mpya anayekwenda kwa jina la jukwaani; Baridi. Sometimes mwaka jana alitoka na wimbo Nipe Nafasi ambao ulienda hewani na kumtambulisha vyema tu kama msanii mwenye uwezo wa kipekee katika kuimba. Yes,yawezekana hukupata nafasi ya kuusikia kwani kama ujuavyo,soko la muziki nalo lina yake. Usijali,unaweza kuusikiliza hapa.
Sasa ili kuthibitisha kwamba uwezo anao na kwamba muziki bado ni chaguo lake kama msanii na njia yake halali ya kuendeleza maisha, Baridi anaachia single yake ya pili. Hii inakwenda kwa jina Ni Wewe ikiwa ni production nyingine kutokea pale Burn Records kwa Sheddy Clever ambaye naye anafanya vizuri katika anga za wapikaji wa muziki.
Usikilize hapa wimbo huu mpya kutoka kwa Baridi…naam Ni Wewe Tu.