Tema mate tuwachape. Kama hujawahi kuambiwa hivyo wakati wa utoto wako,basi ama hukuzaliwa na kukulia Tanzania au umezaliwa kizazi hiki hiki cha .com ambacho badala ya kandambili za kutengeneza mwenyewe wao wanachezea Jordan. Au badala ya kujitengenezea mwenyewe toys unasubiri za kutoka China.
Ulikuwa ni msemo wa kawaida unapotaka kupoza hasira za mtoto….Anakuja anakulilia.Unamwambia nani huyo….tema mate tumchape au tuwachape.Naam ndivyo Madee kutoka Tip Top Connection anavyotukumbusha katika wimbo wake huu mpya…Tema Mate Tuwachape.Usikilize