Hakuna ubishi kwamba Linex ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wenye kipaji cha hali ya juu katika uimbaji na pia katika utungaji wa nyimbo zenye ujumbe wa tofauti hususani kwenye uzingo wa mapenzi ambao artists wengi hupenda kupakimbilia.
Huu hapa ni wimbo wake mpya akiwa amemshirikisha Wyre, msanii kutoka Kenya ambaye sifa zake zinajulikana kote barani Afrika na hata nje ya hapo. Wimbo unaitwa Riziki Yangu.