Quantcast
Channel: Bongo Fleva – Bongo Celebrity
Viewing all 180 articles
Browse latest View live

Vanessa Mdee Anataka “Kurogwa”


“Niroge”-Vanessa Mdee (Official Video)

$
0
0

Vanessa Mdee,Niroge,New Song

Huna haja ya kusubiri zaidi. Video ya wimbo mpya wa Vanessa Mdee uitwao Niroge. Wimbo huu umerekodiwa na Nahreel. Reaction yangu ya kwanza ni kwamba video ni nzuri. Pengine nimeshawahi kuiona video kama hii mahali pengine. Lakini ni nzuri.

Have You Watched NdiNdiNdi Video?

$
0
0

1

It’s probably the most talked about song right now. That comes as a no surprise since it’s from Lady JayDee who, without a doubt, is one of the top artists in the land.

“Migulu Pande”-Madee (Audio)

$
0
0

madee migulu pande

Kuna siku niliwahi kumuulizia msanii fulani wakati wa mazungumzo yangu ya kawaida na Professa Jay(Mbunge wa Mikumi-CHADEMA). Niliuliza, “Hivi jamaa kaacha muziki au?”. Professa akanijibu kwa kifupi, “Hapana, yeye ndio muziki umemuacha”. Kwa mara ya kwanza nikawa nimetambulishwa katika dhana ya mtu kuacha muziki na muziki kumuacha yeye. Ni vitu viwili tofauti.

Kwanini nimeanza kwa utambulisho huo? Madee ni miongoni mwa wasanii ambao hawajaacha muziki na muziki haujamuacha. Alikuwepo na bado yupo. Vijana wengi wamepitia katika himaya yake. Ni jambo la kufurahisha.

Huu hapa ni wimbo wake alioutoa hivi karibuni. Migulu Pande. Sijauelewa sana lakini kuna mengi ambayo siyaelewi siku hizi. Usikilize hapa chini. (Audio Source: DJ Choka)

Tanzanian Court Awards AY & MwanaFA 2.18 Billion Tshs In A Landmark Ruling

$
0
0
FA-AY-pic
A court has awarded two Tanzanian musicians Sh2.18 billion in special damages in a landmark ruling that could set a precedent in the application of the copyright law in the country.
The huge award was won by Bongo flava artistes Ambwene Yessaya “AY” and Hamisi Mwinjuma “MwanaFA” who had sued mobile phone company MIC Tanzania (Tigo), for unauthorised use of their music as caller tunes. A caller tune is a tone that is in the form of music that is heard by a person making a call as they wait for the person being called to answer the phone.
Ilala Senior Resident Magistrate Juma Hassan granted the award on April 11 after a four-year court battle between the parties. The award also includes a separate Sh25 million in general damages.
News of the fine against Tigo only came to light this week on Tuesday when the firm went to the High Court to block the execution of the award pending its appeal. History in the copyright field would be made should the High Court uphold the judgement by the Ilala District Court.
MwanaFA said it was time those who had in the past taken the basic copyright laws for granted realised that things have changed.
“This is a key moment in copyright in Tanzania. This is something that has been happening for quite a long time now mainly because of lack of knowledge and maybe because of the costs associated with such cases,” he said.
He added: “Nobody is supposed to use your work without your permission or agreement and if at all he has benefited then he is supposed to share with you according to the price tag you have set for your work.”
The mobile network operator has, however, filed for a stay of execution and has appealed against the judgment and decree for payment at the High Court. The appeal was initially set to be heard on Tuesday but was adjourned to tomorrow. The artistes claim that Tigo sold without permission in the form of caller tunes content that belonged to them without any agreement between the two parties. The two songs at the centre of the controversy are Dakika Moja and Usije Mjini, which were both done in collaboration by AY and MwanaFA.
Although there are no figures that were mentioned by both sides on the precise income derived from the sale of the two songs, the two artistes believe the company generated revenue.
According to the judgment, the artistes did not have any agreement with anyone to distribute the songs, they did not have an agreement with the defendant (Tigo) and neither did they contract a third party to handle this kind of distribution on their behalf.
The court in its decree states that the defendant infringed the rights of the plaintiffs over their registered joint authorship of musical work and in the process infringed the copyright and/or neighbourhood rights to which civil remedies are applicable.
The court, therefore, ordered the company to pay Sh 5 million as general damages and Sh2.16 billion as special damages in addition to the costs of the suit.
The artistes had in their application asked for damages totalling Sh4.3 billion, claiming that the defendant had generated a significant sum of income through the sale of their two songs to its subscribers across the country.
In recent years, mobile phone operators have been at the centre of a controversy over how much they pay artistes for using their content, with some singers claiming they were not benefiting from their work.
Customised mobile phone caller tunes in Tanzania are largely songs by Bongo Flava artistes.
According to the Journal of Intellectual Property Law and Practice, copyright subsisting in caller tunes and ringtones is similar to copyright protection in any other musical recording, comprising an underlying musical work and a sound recording which are protected under the Copyright Act.
This type of copyright protection in Tanzania is similar to those in South Africa, the United Kingdom, the United States and Jordan.

“Natafuta Kiki”-Raymond Kutoka WCB

$
0
0

Natafuta Kiki+Raymond+Wasafi Records

Yaelekea WCB wameamua kujikita kwenye kujipanua na kukuza vipaji. Baada ya kupata mafanikio kupitia kwa Harmonize, sasa ni zamu ya Raymond. Atoke vipi? Kwa kutizama mazingira vizuri. Siku hizi ukitaka kutoka unafanyaje? Moja ni kupaisha kipaji chako. Mbili ni “Kutafuta Kiki”.

Unaibua issue. Unaongelewa. Instagram na Facebook zinakuwa na hashtag la beef lako. Mitaani watu wakikosa cha kuongelea, jina lako linaokoa jahazi.Mazungumzo yanaendelea.

Ila tatizo moja ninaloliona mara kwa mara kwenye hizi “kiki” ni kwamba kwanza hazina uhusiano na kipato. Kuzungumziwa, kutukanwa au kudhadhalilishwa na bila kuelekea kwa teller(bank) ni upuuzi. Pili ni kwamba unapotafuta “kiki” unahatarisha pia kujipotezea kabisa mashabiki.

Msikilize Raymond akielezea jinsi Kiki zinavyotafutwa au kupatikana. Audio By ChokaMusic

WATCH:”Ibaki Story”-Rich Mavoko (Official Video)

$
0
0

Rich Mavoko Ajiunga na WCB Wasafi na kuachia Ibaki Story

Miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambao tunaweza kukubaliana kwamba wana kipaji cha uimbaji, Rich Mavoko hatuwezi kumweka pembeni. Kipaji anacho. Haishangazi kwamba WCB hivi karibuni wamemuongeza katika orodha yao inayozidi kukua ya wasanii walio chini ya label hiyo.

Rich Mavoko-Ibaki Story WCB

Huu hapa ni wimbo wa kwanza wa Rich Mavoko akiwa chini ya WCB. Unaitwa Ibaki Story.  Pamoja na kipaji cha Mavoko, kitu kimoja ambacho kinaanza kuwa changamoto kwa WCB ni videos. Takribani zote zinafanana. Kuna theme ambayo inaonekana katika video nyingi za hivi karibuni kutoka WCB. Yawezekana ndivyo soko la leo linavyotaka. Binafsi nadhani ubunifu zaidi na utofauti kutoka video moja kwenda nyingine utasaidia lebo hiyo kuendelea kupasua mawimbi kwa mbali zaidi.

 

New Single Alert: “Mama”-Peter Msechu & Banana Zorro

$
0
0
Peter Msechu & Banana Zorro-Mama

Peter Msechu & Banana Zorro-Mama

Kama ilivyo mapenzi, nyimbo zinazohusu Mama zetu kamwe hazipotezi ladha wala nafasi katika burudani. Bila kina-mama, ulimwengu huu haupo. Unaweza kuzungumzia mchango wa kina baba lakini ukweli ni kwamba mchango wa kina mama hauelezeki. Haishangazi kwamba kwenye nyumba Mama anapokuwa namna gani vipi, mambo mengi yanakwenda kombo. Msingi wa mama katika familia sio lelemama.

Mama-Peter Msechu-Banana Zorro

Mama-Peter Msechu & Banana Zorro

Mama ni shujaa. Mama yangu ni shujaa.Mama yako ni shujaa. Mama yake Peter Msechu ni shujaa. Mama yake Banana Zorro hali kadhalika. Hivyo nina furaha kuleta kwako wimbo mpya kutoka kwa Peter Msechu akiwa amemshirikisha Banana Zorro. Wimbo unaitwa Mama. Umeandaliwa na Teaz Villah kutoka Downvilla Records.


Ray C Aingia Tena Rehab

$
0
0

Rehema Chalamila Ray C na matumizi ya madawa ya kulevya

Mara nyingi huwa natamani nisiandike kuhusu kuanguka kwa mtu. Sipendi. Lakini kama kwa kuandika kuhusu kuanguka kunaweza kusaidia aliyeanguka au mwingine ambaye asiposikia ataanguka,basi yatubidi.

Majuzi kwenye mitandao ya kijamii ilisambaa video inayomuonyesha mwanamuziki wa siku nyingi, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C akiwa katika hali ya kusikitisha kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Video hiyo ilimuonyesha akiwa anasaidiwa na Polisi. She was hallucinating. Inadaiwa alikuwa anataka kujidhuru mwenyewe. Ilisikitisha na kuliza wengi. Ray C ni miongoni mwa wanamuziki waliowahi kutamba na bila shaka ana kipaji. Hivi sasa kipaji kinaangamia kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Polisi wale waliokoa maisha yake. Wanastahili pongezi nyingi. Wameitenda kazi yao ya kulinda uhai na usalama wa raia. Wasingejitokeza pale, wakati ule,huenda leo tungekuwa tunaongea mengine.

Ray C goes to rehab

Habari njema ambazo zimepatikana ni kwamba Ray C amepelekwa Life And Hope Rehabilitation Centre (Sober House) iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuachana na matumizi ya madawa hayo. Kituo hicho ndicho ambacho hivi karibuni kilimsaidia mwanamuziki mwingine, Chizi Benz. Baada ya kutoka huko Chidi Benz ameonekana kuwa katika hali nzuri kiafya kiasi cha kuingia mkataba na WCB Wasafi. Ni jambo la kheri.

Kitu kimoja ambacho ni muhimu sana kukikumbuka ni kwamba vita dhidi ya madawa ya kulevya sio ya mtu mmoja. Ni yetu sote. Ray C amewahi kuachana na matumizi. Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliingilia kati na kumsaidia. Ray C akawa Balozi wa kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya. She became vocal and for good reason. Akaanzisha mpaka NGO inayojishughulisha na vita hii nzito. Bila shaka alisaidia wengi wengine.

Nakumbuka hata ujumbe wake kwa Chid Benz pindi ilipojuliana wazi kwamba mwimbaji huyo wa Dar Stand Up alikuwa amefikia kubaya. Leo Chid Benz yupo “clean” na Ray C yupo rehab. Karudia tena. Wengi wanaacha na kisha kujikuta wamerudia tena. Tujiulize kwanini? Tunawapa support ya aina gani wakitoka? Kama jamii tunawaambia nini wanapotoka?

Kiufupi tuna wajibu wa kupiga vita biashara hii kutokea katika kiini chake (kwa wauzaji na wasambazaji). Kuwepo kwa madawa haya mitaani, ni chanzo cha kuendelea kwa matumizi. Yapo.Yanapatikana kirahisi. Wanaomuuzia Ray C na wengine,wapo. Hatuwajui? Ray C hamjui anayemuuzia? Hatujui wanapoyapata? Eeenh…polisi hamjui? Kwanini wananchi tunaishia tu kusema “fulani ni zungu la unga” na kutokwenda mbele kuwataja? Tunaishi nao mitaani. Hatuwajui? Hatuwaoni wakiingia na kutoka?

Serikali inajaribu. Jeshi la Polisi linaonekana kuwa na dhamira fulani katika vita hii. Ni jambo zuri. Ila serikali ilichukulie hili kwa mapana zaidi. Sio la Wizara Ya Mambo Ya Ndani tu. Wizara ya Elimu na Wizara Ya Afya ziungane pia. Utafiti unaonyesha wengi huanza matumizi ya madawa haya wakiwa mashuleni. Wazungu wa unga wanawanyemelea wakiwa mashuleni. Wanaweka kambi pembeni ya mashule. Tupanue vita huko pia. Wanafunzi waelimishwe kuhusu athari na jinsi ya KUSEMA HAPANA.

Vijana wengi wanajiingiza kwenye madawa ya kulevya kutokana na ukosefu wa shughuli maalum za kufanya. Wanakuwa wamekata tamaa. Wengi huanza kama kuonja ili kupunguza msongo wa mawazo (stress). Wengine ni tabia ya kuiga tu. Kitu ambacho hawajui ni kwamba madawa ni “addictive”. Ukianza huwezi kuacha kirahisi. Unakuwa “addicted”.Teja. Wanapomaliza rehab tunawapa muelekeo gani mpya? Tunawapa shughuli za kufanya? Kama ni La… si ni wazi kwamba baada ya muda mfupi tu wanarudia tena?

Chid Benz na Ray C(na hivi karibuni Fanani kutoka HBC) ni wanamuziki wenye majina makubwa. Wanafahamika. Ni rahisi kwao kusaidiwa hata kutokana na michango ya mashabiki zao. Huko mitaani wapo vijana wengi wanaoangamia. Hatuwajui kwa majina wala sura. Lakini ni watoto wa watu,kaka,dada,mjomba,baba,ndugu,rafiki wa wengine. Tuna wajibu. Wewe na mimi.

Ray C kila la kheri.

KIJANA SEMA HAPANA KWA MADAWA YA KULEVYA. FUATA NJIA HIZI.

 

NeW SiNgLe: “Manuari”-Kassim Mganga(Audio)-Produced By Sheddy Clever

$
0
0
Kassim Mganga-Manuari-Produced by Sheddy Clever

Kassim Mganga

Sina shaka kwamba Kassim Mganga ni miongoni mwa vipaji vikubwa vya muziki tulivyonavyo nchini Tanzania. Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia kazi zake na sasa naweza kusema wazi kwamba he’s one of my top favorite artists from motherland. Ninaamini kwenye mpangilio wa mashairi na ladha ya muziki wake.Unbelievable talent.

Hii hapa ni single yake mpya iliyopewa jina “Manuari” ikiwa ni production ya genius producer,Sheddy Clever kutoka Burn Records.

Kassim Mganga-Manuari Produced By Sheddy Clever-Burn Records

Kassim Mganga-Manuari Produced By Sheddy Clever-Burn Records

Kassim Mganga ambaye anajiita Tajiri wa Mahaba, anaendeleza simulizi nzuri ya kimapenzi ambayo kama huna uelewa wa haraka wa lugha ya Kiswahili itabidi usikilize zaidi ya mara moja kuielewa.Ukishaielewa utaiweka kwenye auto-replay. Twende…

“Hewala”-Linex Feat. Christian Bella (New Joint)

$
0
0

Linex-Christian Bella-Hewala

Linex and Christian Bella are two heavyweights vocalists. One hails from Kigoma. The other is from DRC. He consider Tanzania to be his home for now. Anyone who brings to the land such a talent is welcomed.(you know). They are hereby collaborating in a song titled Hewala. Listen below(support them for finishing the legal download). You can also listen to the audio version posted here.

“Kipenda Roho”-Rama Dee (ViDeO)

$
0
0

Rama Dee-Kipenda Roho-Video

Rama Dee is crazily talented. One of the best vocalists. The first I heard him was in Dar. I had got a ride from one of my partners in crime, Othman. Enjoying the rare rides where I get to be a passenger, the song “Kama Huwezi” featuring Lady Jaydee came on. I didn’t know who he was. Othman happened to be his number one fan too. Long story short, we kept that song on repeat. The usual traffic jams of Dar didn’t bother us. I became a fan.

Few months later I got in touch with him encouraging him to never stop doing music. He was in Australia. I am glad he listened. Not to suggest he was about to quit.Nah. I just felt we need to hear a lot more from him. Here is one his latest songs, Kipenda Roho. The video is simple yet unique from what I constantly see. He didn’t go far to South Africa..I guess…Watch

20 Percent Kurejea Tena Chini Ya Kombinega Sound

$
0
0
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann  Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.(Picha na Sultani Kipingo)

Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.(Picha na Sultani Kipingo)

Kama kuna msanii alizipaisha tuzo za muziki za Kili (Kilimanjaro Music Awards) mwaka 2011 basi msanii huyo ni 20% (Twenty Percent). Alinyakua tuzo tano kwa mpigo. Ilikuwa historia. Baada ya ushindi ule, Twenty Percent akapotea. Alipoibuka ilikuwa ni aidha amekamatwa na madawa ya kulevya au lingine ambalo halikumsaidia. Akawapisha wengine. Mwenyewe anasema aliamua kwenda kulima. Yote heri.

Yote ameamua kuyaweka kando. Anarejea. Kwa mujibu wa blog ya Ankal Michuzi, Twenty Percent anarejea akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya Kombinega inayoendeshwa na producer wa siku nyingi, John Shariza almaarufu kama Mann Water.

Twenty Percent Akisaini Mkataba

Twenty Percent Akisaini Mkataba

Katika hafla fupi ya kutiliana sahihi iliyofanyika katika ofisi/studio za Combination Sound zilizopo Kinondoni Mkwajuni, imewekwa wazi kwamba 20% anajiandaa kutoa album yake mpya itakayoitwa Sauti ya Gharama. Single ya kwanza kutoka kwenye album hiyo itatoka tarehe 18 mwezi huu.
Tunasubiri kwa hamu ujio mpya wa Twenty Percent.

 

“Matatizo”-Harmonize From WCB(Official Video)

$
0
0

Harmonize-Matatizo-WCB

Kila binadamu hukumbwa na matatizo. Kuna ya muda mfupi na kuna yale ambayo huweza kukuandama kwa miaka nenda rudi. Yanaganda kama mdudu ruba. Maisha bila matatizo hayapo. Masikini wana matatizo yao na matajiri wana yao. Pengine ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotaka. Kuna watu wangekuwa hawashikiki.

Nafurahi kwamba katikati ya nyimbo lukuki za mapenzi, Harmonize ameamua kuimba kitu tofauti. Kitu ambacho kila mtu anaweza kuhusiana nacho.

Ila jambo moja ambalo ningependa kuligusia hapa ni kwamba ukubwa au udogo wa tatizo unategemea na jinsi unavyolitizama. Matatizo ni fursa pia. Liangalie tatizo kwa mrengo tofauti na utaona kila kitu kinabadilika. Ndio maana, Mungu hakupi mtihani ambao anajua hutouweza.La Hasha! Anakupa mitihani ya saizi yako. Itizame kwa makini, utaona fursa kedekede.

Huu hapa Matatizo kutoka kwa Harmonize aliyepo WCB.

“Sawa”- Shaa (BrAnD NeW)

$
0
0

Shaa-Sawa-Wimbo-Mpya

Kuna kitu ambacho kinanivutia sana kuhusu muziki kutoka kwa Shaa hususani tangu alipoamua kufanya muziki ambao mimi nauita “wa kwetu”. Ni aina fulani ya muziki ambayo naamini kama tungeamua kuipa nafasi isingetulaza kama tumekunywa klorofomu.

Ila hayo tutatafuta muda tuyaongelee. Ngoja kwanza nawe usikilize “Sawa” kutoka kwa Shaa. Sawa eenh!


“Waache Waoane”-Chege Ft.Diamond Platinumz

$
0
0

Waache-Waoane-Chege-Diamond-Platinumz

As Friday looms, we thank God it is here. Music is always a great company. The new joint is even better. Talking about new joint here is a new one from Chege featuring Diamond Platinumz. Waache Waoane is the name of the song. Literal translation; Let Them Marry Each Other.

#TBT: “Hii Leo”-East Coast Team

$
0
0
East Coast Team,Upanga,Dar-es-salaam

The East Coast Team

Leo naanzisha kipengele kipya. Kila Alhamisi nitakuwa natupia nyimbo,video nk kutoka katika harakati za mwanzo za Bongo Fleva/Hip-Hop na pia muziki wa Afrika kwa ujumla bila kusahau ile kutoka ughaibuni au Marekani ambayo kwa njia moja au nyingine ilisaidia kuibua “za kwetu”. Tutakuwa na Throw Back Thursday(TBT). Zamani tuliita “Zilipendwa”. Bado zipo za kale nyingi sana kwenye blog hii. Andika tu kwenye search button juu kulia “Zilipendwa”. Nakuhakikishia utafurahi na roho yako.

Baadhi ya hizi nyimbo ndizo zilitengeneza njia kufikia hapa ulipo muziki wa Tanzania. Naelewa bado tunahangaika kupata authentic Tanzanian music. Naamini tutafika. Tulipotoka sio mbali sana. Taifa letu bado ni changa ukilinganisha na mengine. The struggle is real.

Hii hapa ni Hii Leo kutoka East Coast Team vijana waliokuwa na makazi yao mitaa ya Upanga jijini Dar-es-salaam. East Coast team iliundwa na vijana wengi wakiwemo Crazy GK, AY,MwanaFA,Abbas nk. MwanaFA na AY waliendelea kivyao baadae na kuwa na mafanikio makubwa. Lakini hawajawahi kuondoka East Coast. Mara kwa mara pamekuwa na tetesi za East Coast kurudiana na kutoa project ya pamoja. Tunasubiri.

Wacheki hapa kwenye wimbo wao Hii Leo

VIDEO: “Natafuta Kiki”-Raymond (WCB)

$
0
0

Natafuta Kiki-WCB-Raymond

Hii hapa ni video mpya kutoka WCB kwa msanii Raymond. Wimbo huu unaoitwa Natafuta Kiki ni production ya Lizer Classic kutoka Wasafi Records. Wimbo umeandikwa na Raymond huku video ikiwa ni kazi ya Kwetu Studio

 

“Maumivu”-Esaya

$
0
0

esaya

On a daily basis, we receive many new songs/artists requests for publication of their content. I wish I could keep up with everything sent in. I can’t. However, I try to listen to everything sent in. There are lots of talents out there. There are surprises. I mean surprise in a bad way. You listen and go WTF. Who took this man/woman into a studio? Trust me; I get a lot of those.

Among listenable stuff, here is Maumivu by Esaya. You may not have heard about him before. I understand. Keep watching and listening. Moreover, listen to this one. The details are on the image above.

Lady Jaydee – Sawa Na Wao (Official Music Video)

$
0
0

Lady Jaydee,Sawa Na Wao,Official video

Back in the 90s, Judith Wambura emerged as one of few female artists in Tanzania. The “movement” of the new generation music had started. I am not sure if we referred her as “Lady” then. She understood that haste makes waste. Slowly but steadily the lady we now know as Lady Jaydee became dominant.

When I look back and ask myself how has she maintained her position even in the industry full men, the simple answer could be “knowing thyself.” She knows who she is. Those who thought she is a sitting target have come to realize they were/are wrong.

The fans have showered her with different names including “Commando.” They refer to her toughness to fight injustice, sexism and all the above. Among multiple names, however, Lady Jaydee suits her life and persona.

Under Rockstar4000 Management, here is the official video for her latest single titled Sawa Na Wao. The notes from publication reads;

‘Sawa Na Wao’ is all about life, love, relationships and portraits life through the lens of a relationship and some of those temptations distractions that often disrupts or destroy those relationships. Lady Jaydee’s next smash hit release through her exclusive worldwide partnerships with her record label and management company ROCKSTAR4000, publishing collaboration with ‘Rockstar Publishing’ and Content Partnership with RockstarTV.

The ‘Sawa Na Wao’ music video was Directed by the phenomenal Director Meji.

You can watch it below

 

Viewing all 180 articles
Browse latest View live