Quantcast
Channel: Bongo Fleva – Bongo Celebrity
Viewing all articles
Browse latest Browse all 180

20 Percent Kurejea Tena Chini Ya Kombinega Sound

$
0
0
Msanii Abbas Hamisi Kinzasa almaarufu kama 20% (Twenty per Cent) wakipongezana na producer nguli wa muziki nchini John Shariza a.k.a Mann  Water baada ya kuwekeana saini mkataba wa kufanya kazi pamoja chini ya lebo ya KOMBINENGA kwenye studio za Combination Sounds Kinondoni Studio jijini Dar es salaam.(Picha na Sultani Kipingo)

Kama kuna msanii alizipaisha tuzo za muziki za Kili (Kilimanjaro Music Awards) mwaka 2011 basi msanii huyo ni 20% (Twenty Percent). Alinyakua tuzo tano kwa mpigo. Ilikuwa historia. Baada ya ushindi ule, Twenty Percent akapotea. Alipoibuka ilikuwa ni aidha amekamatwa na madawa ya kulevya au lingine ambalo halikumsaidia. Akawapisha wengine. Mwenyewe anasema aliamua kwenda kulima. Yote heri.

Yote ameamua kuyaweka kando. Anarejea. Kwa mujibu wa blog ya Ankal Michuzi, Twenty Percent anarejea akiwa msanii wa kwanza kusaini mkataba na lebo mpya ya Kombinega inayoendeshwa na producer wa siku nyingi, John Shariza almaarufu kama Mann Water.

Twenty Percent Akisaini Mkataba

Twenty Percent Akisaini Mkataba

Katika hafla fupi ya kutiliana sahihi iliyofanyika katika ofisi/studio za Combination Sound zilizopo Kinondoni Mkwajuni, imewekwa wazi kwamba 20% anajiandaa kutoa album yake mpya itakayoitwa Sauti ya Gharama. Single ya kwanza kutoka kwenye album hiyo itatoka tarehe 18 mwezi huu.
Tunasubiri kwa hamu ujio mpya wa Twenty Percent.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 180

Trending Articles