Kila binadamu hukumbwa na matatizo. Kuna ya muda mfupi na kuna yale ambayo huweza kukuandama kwa miaka nenda rudi. Yanaganda kama mdudu ruba. Maisha bila matatizo hayapo. Masikini wana matatizo yao na matajiri wana yao. Pengine ndivyo Mwenyezi Mungu alivyotaka. Kuna watu wangekuwa hawashikiki.
Nafurahi kwamba katikati ya nyimbo lukuki za mapenzi, Harmonize ameamua kuimba kitu tofauti. Kitu ambacho kila mtu anaweza kuhusiana nacho.
Ila jambo moja ambalo ningependa kuligusia hapa ni kwamba ukubwa au udogo wa tatizo unategemea na jinsi unavyolitizama. Matatizo ni fursa pia. Liangalie tatizo kwa mrengo tofauti na utaona kila kitu kinabadilika. Ndio maana, Mungu hakupi mtihani ambao anajua hutouweza.La Hasha! Anakupa mitihani ya saizi yako. Itizame kwa makini, utaona fursa kedekede.
Huu hapa Matatizo kutoka kwa Harmonize aliyepo WCB.