Quantcast
Channel: Bongo Fleva – Bongo Celebrity
Viewing all articles
Browse latest Browse all 180

#TBT: “Hii Leo”-East Coast Team

$
0
0
East Coast Team,Upanga,Dar-es-salaam

The East Coast Team

Leo naanzisha kipengele kipya. Kila Alhamisi nitakuwa natupia nyimbo,video nk kutoka katika harakati za mwanzo za Bongo Fleva/Hip-Hop na pia muziki wa Afrika kwa ujumla bila kusahau ile kutoka ughaibuni au Marekani ambayo kwa njia moja au nyingine ilisaidia kuibua “za kwetu”. Tutakuwa na Throw Back Thursday(TBT). Zamani tuliita “Zilipendwa”. Bado zipo za kale nyingi sana kwenye blog hii. Andika tu kwenye search button juu kulia “Zilipendwa”. Nakuhakikishia utafurahi na roho yako.

Baadhi ya hizi nyimbo ndizo zilitengeneza njia kufikia hapa ulipo muziki wa Tanzania. Naelewa bado tunahangaika kupata authentic Tanzanian music. Naamini tutafika. Tulipotoka sio mbali sana. Taifa letu bado ni changa ukilinganisha na mengine. The struggle is real.

Hii hapa ni Hii Leo kutoka East Coast Team vijana waliokuwa na makazi yao mitaa ya Upanga jijini Dar-es-salaam. East Coast team iliundwa na vijana wengi wakiwemo Crazy GK, AY,MwanaFA,Abbas nk. MwanaFA na AY waliendelea kivyao baadae na kuwa na mafanikio makubwa. Lakini hawajawahi kuondoka East Coast. Mara kwa mara pamekuwa na tetesi za East Coast kurudiana na kutoa project ya pamoja. Tunasubiri.

Wacheki hapa kwenye wimbo wao Hii Leo


Viewing all articles
Browse latest Browse all 180

Trending Articles