Kama ilivyo mapenzi, nyimbo zinazohusu Mama zetu kamwe hazipotezi ladha wala nafasi katika burudani. Bila kina-mama, ulimwengu huu haupo. Unaweza kuzungumzia mchango wa kina baba lakini ukweli ni kwamba mchango wa kina mama hauelezeki. Haishangazi kwamba kwenye nyumba Mama anapokuwa namna gani vipi, mambo mengi yanakwenda kombo. Msingi wa mama katika familia sio lelemama.
Mama ni shujaa. Mama yangu ni shujaa.Mama yako ni shujaa. Mama yake Peter Msechu ni shujaa. Mama yake Banana Zorro hali kadhalika. Hivyo nina furaha kuleta kwako wimbo mpya kutoka kwa Peter Msechu akiwa amemshirikisha Banana Zorro. Wimbo unaitwa Mama. Umeandaliwa na Teaz Villah kutoka Downvilla Records.